Psalms 18:20-24


20 a Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu;
sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.
21 bKwa maana nimezishika njia za Bwana;
sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.
22 cSheria zake zote zi mbele yangu,
wala sijayaacha maagizo yake.
23 dNimekuwa sina hatia mbele zake,
nami nimejilinda nisitende dhambi.
24 e Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu;
sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake.
Copyright information for SwhNEN